Wanawake Wengi Wanaojiuza Maeneo ya Manzese ni Wake za Watu

Wednesday, May 12, 2010 / Posted by ishak /

IMEDAIWA kuwa wanawake wengi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao katika maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam ni wake za watu na imegundulika kuwa wanaagizwa na waume zao wakafanye biashara hiyo ili wapate pesa za kujikimu.
Hayo yamegundulika katika utafiti wa kina uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Madawa Afrika [AMREF]

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Meneja wa Mradi wa Haki za Wananchi wa taasisi hiyo, Michael Kimaryo, wakati wa semina iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari za Ukimwi (AJAAT) kwa kushirikiana na taasisi hiyo.

Kimaryo alisema walibaini hali hiyo wakati walipokuwa wakifanya ufuatiliaji kuhusu mradi huo uliolenga kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya afya ya ukimwi na mambo mengine katika maeneo ya Manzese, Tandale na Kiwalani, Vingunguti na kwingineko

Alisema wanawake hao wamejiingiza katika biashara hiyo ambayo waume zao majumbani wanatambua hali hiyo na huwaruhusu ili waweze kujipatia kipato cha siku cha kujikimu na familia zao.

Mradi huo wa AMREF ulianzishwa mwaka 2008 ukiwa na lengo la kuwakomboa wananchi katika nyanja mbalimbali, kuwaelimisha kuhusiana na ugonjwa wa ukimwi na jinsi ya kujikinga na walioathirika kujifunza njia za kuepuka kuwaambukiza wengine.

Mradi huo ulilenga zaidi maeneo ya Manzese na Tandale.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment