Uchungu wa Mwana Aujuaye ni....

Wednesday, May 12, 2010 / Posted by ishak /


Siku zote husemekana kuwa akina mama kutokana na uchungu kwa watoto wao huwa tayari kuyatoa maisha yao kwaajili yao, lakini pia akina baba nao si wa kubeza kama baba huyu wa nchini Australia ambaye alitumia mwili wake kama ngao ya kumlinda mtoto wake na mzinga mkubwa wa gari.
Andrew Leach alikuwa amebeba mtoto wake wa miezi minne akitembea pamoja na familia yake pembeni ya barabara wakati gari lililokuwa likiendeshwa na bibi lilipopoteza muelekeo na kumgonga.

Ajali hiyo mbaya ilitokea magharibi mwa jiji la Sydney kwenye kitongoji cha Penrith.

Video za kamera ya ulinzi zililinasa tukio hilo ambapo Leach alitumia mwili wake kama ngao ya kumlinda mtoto wake na mzinga mkubwa wa gari uliotokea.

"Wakati wa ajali nilifikiria, kama gari lingenigonga mgongoni, lingenivunja mguu au kiungo chochote kile ningeweza kupona lakini kama lingemgonga mtoto wangu asingepona", alisema Leach.

Leach alimshikilia mtoto wake kifuani na aliendelea kumshikilia wakati wa gari lilipomgonga na kumburuza kwenye kiambaza cha ukuta wa duka huku miguu yake ikiwa imebanwa ukutani.

Mtoto wake alinusurika kwenye ajali hiyo na hakupata jeraha lolote lile.

Leach alivunjika miguu yake yote miwili wakati wazazi wake aliokuwa akitembea nao wakati wa ajali, walijeruhiwa vibaya sana lakini hivi sasa hali zao zinaendelea vizuri.

Ajali hiyo ilitokea mwaka 2008 lakini habari kuhusiana na ushujaa wa Leach kumuokoa mwanae zimetolewa wiki hii na televisheni ya 9 TV ya Australia.


source nifahamishe