Autoa Sadaka Ulimi Wake Ili Apate Mtoto

Monday, February 08, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja wa nchini India ambaye pamoja na jitihada zake zote alishindwa kupata mtoto katika ndoa yake ya miaka minne, aliamua kuukata ulimi wake na kuutoa sadaka kwa miungu ya kihindi.
Mukesh Kumar mkazi wa kijiji cha Banthari katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India, ameamua kuutoa kafara ulimi wake baada ya kushindwa kupata mtoto katika ndoa yake ya miaka minne.

Kumar ambaye siku zote amekuwa akigoma kwenda hospitali kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo, aliamua kwenda kwenye mahekalu ya miungu wa kihindu na kuutoa kafara ulimi wake.

Kumar alikuwa akiamini kuwa iwapo atautoa kafara ulimi wake kwa mungu wa kihindu anayeitwa Shiva basi atapata mtoto.

Hata hivyo kitendo chake cha kukikata kipande kikubwa cha ulimi wake kilimsababishia maumivu makali pamoja na kusababisha hali yake iwe na mbaya kiasi cha watu waliokuwa karibu yake kuamua kumwahisha hospitali.

Madaktari walifanikiwa kukiunganisha tena kwa njia ya operesheni kipande cha ulimi wake ambacho awali Kumar alikitoa kafara kwa matumaini ya kupata mtoto.

source nifahamishe