Mwanaume Aliyetuhumiwa Uchawi Auliwa Kwa Mabomu

Thursday, February 11, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja wa nchini Burundi aliyekuwa akituhumiwa kuwaroga ndugu zake, amefariki dunia pamoja na familia yake baada ya bomu kurushwa ndani ya nyumba yake.
Mwanaume huyo alifariki dunia pamoja na watoto wake watatu wakati bomu liliporushwa na kulipuka ndani ya nyumba yake.

Tukio hilo lilitokea jioni ya siku ya jumanne katika kijiji cha Itaba kilichopo ukanda wa kati wa Burundi.

Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Emmanuel Nyandwi aliuliwa baada ya kutuhumiwa kumroga mmoja wa ndugu zake na kupelekea kifo chake.

Bomu hilo lilirushwa jikoni kwake wakati Nywandwi alipokuwa amekusanyika na mkewe na watoto wake watatu wenye umri kati ya miaka 7 na 15.

Mabomu yanapatikana kirahisi nchini Burundi na hununuliwa kwa Tsh. elfu moja tu na hutumika zaidi kwenye kutatua migogoro ya ardhi.

Mwaka 2008 pekee watu 130 walifariki dunia baada ya kulipukiwa na mabomu.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment