Aweka Rekodi Ya Kumeza Majambia 18

Tuesday, February 09, 2010 / Posted by ishak /


Mfanya shoo za mitaani wa nchini Australia ameweka rekodi ya dunia kwa kumeza majambia 18 kwa wakati Chayne Hultgren, mfanya shoo za mitaani wa nchini Australia mwenye umri wa miaka 31, ameingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia baada ya kufanikiwa kumeza majambia 18 kwa wakati mmoja.

Chayne alifanikiwa kuweka rekodi hiyo kwa kuyaingiza tumboni mwake majambia 18 yenye makali kama kiwembe ambayo yote yalikuwa na urefu wa sentimeta 72.

Chayne ambaye ni maarufu kwa jina la "Space Cowboy" aliivunja rekodi aliyoiweka yeye mwenyewe mwaka 2008 alipomeza majambia 17.

Chayne anawaonya watu wanaotaka kuvunja rekodi yake kuwa yeye alijiandaa miaka mingi sana kuweza kuweka rekodi hii.

Chayne anasema kuwa alianza usanii wa kumeza majambia alipokuwa na umri wa miaka 16 alipofanikiwa kulimeza jambia moja.

"Nimekuwa nikijiandaa kuweka rekodi hii tangia nilipokuwa na umri wa miaka 16", alisema Chayne.

source nifahamishe