MIUJIZA nchini Haiti, Aokolewa Siku ya 27 Baada ya Kuzikwa na Kifusi

Tuesday, February 09, 2010 / Posted by ishak /


Miujiza imetokea nchini Haiti kwa mwanaume ambaye alikuwa hana chakula wala maji kuweza kuokolewa toka kwenye kifusi cha jumba alilokuwemo siku 27 baada ya kufunikwa na kifusi cha jengo hilo wakati tetemeko kubwa la ardhi lilipotokea nchini Haiti.
Madaktari nchini Haiti wanampatia matibabu mwanaume mwenye umri wa miaka 28 wa nchini Haiti ambaye ameokolewa toka kwenye kifusi cha jengo alilokuwemo siku 27 baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuikumba Haiti januari 12 mwaka huu.

Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Evans Monsigrace, aliokolewa jana jumanne na aliwaambia madaktari kuwa alifunikwa na kifusi cha nyumba aliyokuwemo wakati alipokuwa akipika wali.

"Kimaajabu ameweza kuishi 27 chini ya kifusi cha nyumba yake", alisema daktari Dushyantha Jayaweera, mganga mkuu wa hospitali aliyolazwa mwanaume huyo.

Kwa mujibu wa mama yake Evans, Evans aliokolewa baada ya kugunduliwa na watu waliokuwa wakiondoa kifusi cha nyumba hiyo.

Dokta Jayaweera alisema kuwa Evans alioneka kuwa dhoofu sana na kama amechanganyikiwa vile lakini ogani zake zote zilionekana kuwa salama.

Evans aliwaambia madaktari kuwa aliishi chini ya kifusi kwa muda wote huo bila maji wala chakula na kuwafanya madaktari watume wataalamu kwenye eneo alilookolewa kuthibitisha madai yake.

Wataalamu hao walishindwa kugundua uwepo wa maji au chakula kwenye eneo hilo na kuwafanya madaktari waumize vichwa wasijue imekuwaje Evans ameweza kuishi siku zote hizo bila kula wala kunywa maji.

"Tukio lake limetufanya tuanze kufikiria upya yale tuliyokuwa tukiyajua kuhusiana na mwili wa binadamu", alisema dokta Jayaweera.

source nifahamishe