Mtoto wa Miaka 9 Ajifungua Mtoto

Monday, February 08, 2010 / Posted by ishak /


Msichana mwenye umri wa miaka 9 wa nchini China ameingia kwenye rekodi ya akina mama wenye umri mdogo sana duniani baada ya kujifungua mtoto wa kike mwenye uzito wa kilo 2.7.
Msichana huyo mwanafunzi mwenye umri wa miaka 9 alijifungua mtoto wake wa kike kwenye hospitali moja katika mji Changchun, katika jimbo la Jilin nchini China.

Msichana huyo alijifungua mtoto huyo kwa njia ya operesheni wakati mimba yake ikiwa na muda wa miezi minane na nusu.

Gazeti la The City Evening News la nchini China limeripoti kuwa msichana huyo na mwanae wote wana afya njema hivi sasa lakini wazazi wa msichana huyo wamepeleka malalamiko yao polisi.

Kwa mujibu wa sheria za China, kujamiiana na mtoto mwenye umri chini ya miaka 14 kunahesabika kama kosa la ubakaji.

Msichana huyo wa China ameingia kwenye orodha ya akinana mama wa duniani wenye umri mdogo sana. Msichana mwenye umri mdogo kuliko wote duniani kujifungua mtoto ni Lina Medina, wa nchini Peru, ambaye alijifungua mtoto akiwa na umri wa miaka mitano mwaka 1939.

Serikali ya China imekuwa ikiendesha kampeni nchi nzima kupunguza idadi ya mimba katika umri mdogo kwa kuzipiga marufuku tovuti zote zenye picha au video za ngono.

Wanafunzi wa shule za sekondari wamekuwa wakisimamishwa shule wanapogundulika wanajihusisha na vitendo vya ngono.

Hata hivyo kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaotoa mimba kiasi cha kwamba hospitali moja ya mjini Shanghai ilisema kuwa theluthi ya wanawake wanaotoa mimba kwenye hospitali hiyo ni wanafunzi.

source nifahamishe