Balozi mmoja wa nchi za kiarabu amempa talaka mkewe mpya muda mfupi baada ya kuoana naye baada ya kuiona sura yake kwa mara ya kwanza baada ya hijabu kufunuliwa na kugundua kuwa mkewe huyo mpya ana makengeza na ana vinyweleo usoni.
Balozi mmoja katika nchi za kiarabu jina kapuni alizivunja sherehe za harusi baada ya kuiona sura ya mkewe kwa mara ya kwanza muda mfupi baada ya kufunga naye ndoa na kugundua ana makengeza na vinyweleo kwenye kidevu chake (ndevu za wanawake).
Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News balozi huyo alikuwa akikutana na mwanamke huyo mara chache sana kabla ya siku ya harusi na wakati wote mwanamke huyo alikuwa akiufunika uso wake kwa Niqab (Vazi linalofunika uso na kuacha macho pekee wazi).
Baada ya ndoa kufungishwa balozi huyo alitaka kumbusu mkewe na ndipo alipofanikiwa kuiona sura yake kwa mara ya kwanza na kugundua ana vinyweleo kwenye kidevu na ana macho yenye makengeza.
Balozi huyo alikata shauri la kuivunja ndoa hiyo kwenye mahakama ya sharia za kiislamu katika falme za kiarabu akisema kuwa aliingizwa mkenge wa ndoa na mama wa mwanamke huyo baada ya kuonyeshwa picha za dada yake badala ya zake.
Balozi huyo alitaka ndoa hiyo ivunjwe na pia alimtaka mwanamke huyo amlipe fidia ya dirham 500,000 kwa mikufu, nguo na zawadi zingine alizomnunulia.
Mahakama ilikubali kuivunja ndoa hiyo lakini ilitupilia mbali madai ya fidia ya balozi huyo.
Taarifa iliyotolewa haikutaja jina la balozi huyo na wala haikutoa maelezo zaidi kuhusiana na sakata hilo.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment