VILIO simanzi vilitawala jana katika viwanja vya Mahakama ya Rufani baada ya Jaji Neema Chusi kutangaza kuwaachia huru watoto wawili wa Nguza Viking kwa kile alichosema walifungwa kimakosa na hawakuhusika katika kesi ya msingi .
Hukumu hiyo iliyoanzwa kusomwa saa 3 za asubuhi jana, ambapo umati mkubwa wa watu kutoka kona mbalimbali za jijini Dar es Salaam na wanamuziki mbalimbali nchini walifurika kushuhudia hatma ya rufaa ya wanamuziki hao waliyowsilisha katika mahakama hiyo.
Katika mashitaka ya kubaka Jaji Chusi alisema kuwa, jopo lililokuwa likisikiliza rufani hiyo limebaini kuwa, katika mashitaka 10 ya kubaka yaliyokuwa yakiwakabili wafungwa hao Francis Nguza na mdogo wake Mbangu Nguza hawakuhusika nalo kabisa.
Alisema kuwa ushahidi unaonesha wazi kuwa wakati makosa hayo yakitendeka mtoto mmoja alikuwa shuleni na mwenzake alikuwa ziarani mikoani.
Na kusema kuwa upande wa mashitaka uliowasilishwa katika Mahakama ya Kisutu haikufuata sheria juu ya ushahidi uliotolewa kama kosa la kubaka lililokuwepo mahakamani kwakuwa haikuwepo PF 3 toka Hospitali ya Mwananyamala kwa maelezo.
Aliongeza kuwa japo ushahidi wa mshitakiwa una mapungufu lakini ushahidi uliotolewa na Dk.Pretoria Ngeloi alidai kuwa, baadhi ya watoto waliobakwa na wanamuziki hao walikutwa na maambukizi ya ugonjwa wa gono.
Alisema kuwa ushahidi uliotolewa kwa pande zote mbili ziliridhika na washitakiwa walihusika kwa makosa ya kubaka na kulawiti.
Hivyo majaji waliona kuwa katika mashitaka hayo Babu Seya na Papii Kocha waliyatenda wote kwa pamoja na watoto hao wawili hawakuhusika katika ubakaji huo.
Akitoa hukumu hiyo Chusi alisema kuwa washitakiwa hao walipatikana na mashitaka 5 ambapo mashitaka 11 ya kulawiti alisema kuwa, walibaini kuwa wafungwa hao wote hawakuyatenda bali yalitungwa kwa nia ya kuwakandamiza zaidi.
Kutokana na kauli hiyo Babu Seya na wanawe walianza kuangua vilio na familia ya mwanamuziki huyo hali iliyosababisha ndugu, jamaa na watu waliofurika mahakamani hapo kuanza kuangua vilio kwa kauliu hiyo ya Jaji Chusi.
Hivyo wafungwa hao ambao walishaanza nklutumiki kifungo hicho jana waligonga mwamba dhidi ya rufani yao na wameruishwa kwenda kutumikia kifungo hicho tena.
Baadhi ya watu waliweza kuhojiwa na NIFAHAMISHe alisem kwu wanaiomba serikali kuweza kuangalia zaidi sakata hilo kwani hata kuachiwa kwa watoto hao ni huzuni kwa kuwa mzazi wao ambao ni tegemeo lao amerudishwa gerezani.
Kwa upande wa mawakili wanaowatetea wafungwa hao waliiomba mahakama iwachie huru wanamuziki hao kwa kuwa hukumu iliyowatia hatiani ilikuwa na dosari nyingi za kisheria.
Pia walidai kuwa kesi hiyo ilikuwa ya kupangwa na kwamba hawajawahi kuona hukumu ya hovyo ya aina hiyo tangu waanze kufanyakazi ya uwakili kwa zaidi ya miaka 30 sasa.
Katika kesi ya msingi wasanii hao walikuwa wakituhumiwa kutenda makosa kumi ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya Aprili na Oktoba mwaka 2003 maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment