Msanii wa Marekani Awabaka na Kuwazalisha Binti Zake Watoto Sita

Friday, March 12, 2010 / Posted by ishak /


Mkurugenzi wa kutengeza video za muziki wa Marekani ambaye alitengeneza video ya wimbo maarufu 'Killing me softly' wa kundi la Fugees ametiwa mbaroni kwa kuwabaka na kuwazalisha watoto sita binti zake watano.
Aswad Ayinde, au maarufu kama Charles McGill ambaye alitengeneza video ya ‘Killing Me Softly,’ ya kundi la Fugees la Marekani ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuwabaka binti zake watano na kuwazalisha watoto sita katika kipindi cha miaka 22 kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 2002.

Ayinde anadaiwa kumwambia mkewe na watoto wake kuwa mwisho wa dunia umekaribia na watakaonusurika ni yeye, wanae na watu wengine walioteuliwa.

Ayinde aliiambia familia yake kuwa ili kulinda kizazi chake damu yake isichafuliwe inabidi afanye nao mapenzi na wazae watoto kutoka kwa damu yake mwenyewe.

Kali zaidi ni kwamba baada ya kuwatia mimba binti zake watatu, aliwazalisha yeye mwenyewe na watoto waliozaliwa hawakusajiliwa majina yao serikalini.

Ayinde anakabiliwa na jumla ya mashtaka 27 ambapo kila binti yake mmoja amemfungulia kesi ya mashtaka matano. Makosa mengine amefunguliwa na mkewe wa zamani.

Mke wa zamani wa Ayinde anayeitwa Beverly ambaye alizaa na Ayinde watoto tisa, alitoa ushahidi wa Ayinde kuwabaka binti zake na alielezea jinsi Ayinde alivyokuwa akimpiga yeye na watoto wake kwa kutumia mbao.

"Nilijua alichokuwa akifanya lakini nilishindwa kusema chochote kwa kuhofia kipigo", alisema mke huyo wa zamani wa Ayinde ambaye alinusurika maisha yake baada ya kufanikiwa kutoroka toka kwenye nyumba ya Ayinde.

Ayinde mwenye umri wa miaka 51 anashikiliwa na polisi na atapandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mwezi ujao.

Enzi zake Ayinde alifanikiwa kuzawadiwa tuzo ya MTV kwa kuitengeneza vizuri sana video ya wimbo wa Fugees.

source facebook