Amuua Mkewe Baada ya Kunyimwa Unyumba

Saturday, July 24, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja wa nchini Uingereza ambaye alikuwa akipenda sana kuliko kawaida kupewa unyumba na mkewe, amemuua mkewe baada ya mkewe kumnyima unyumba.
Brent Mott mwenye umri wa miaka 32 alimuaa mkewe, Kate, mwenye umri wa miaka 35 baada ya mkewe huyo kulalamika kwa marafiki zake na wafanyakazi wenzake kuwa amechoka kudaiwa unyumba kila wakati na mumewe.

Kabla ya siku ya tukio hilo, Mott alikuwa amepigwa marufuku na mahakama kuingia kwenye chumba cha mkewe baada ya wanandoa hao kuamua kuivunja ndoa yao.

Mott alimuua Kate siku moja kabla ya mahakama kutoa hukumu ya kuvunja ndoa yao ambapo Mott angetakiwa ahame nyumba na kumuacha Kate na watoto wao wawili.

Siku ya tukio hilo januari 21 mwaka huu, Mott alimfuata mkewe bafuni wakati akioga na kumuomba unyumba, alipokataliwa aliamua kutumia pijama ya mkewe kumnyonga.

"Baada ya kumuua mkewe alimvalisha nguo zingine na kumuingiza kwenye gari la familia na kumpeleka kwenye eneo la mashamba ambapo aliligongesha gari hilo ili kufanya ionekane mkewe amefariki kwa ajali", alisema mwendesha mashtaka Nigel Power akiiambia mahakama mjini Liverpool.

"Siku iliyofuatia alizuga hajui mkewe alipo na kuwapigia simu wakwe zake na polisi akisema anahofia kupotea kwa mkewe", aliendelea kusema mwendesha mashtaka huyo.

Mott ambaye ni mkazi wa Merseyside, alituhumiwa kuwa alikuwa akimnyanyasa sana mkewe kwa unyumba kiasi cha kufikia kudai unyumba siku tano baada ya mkewe kujifungua mtoto kwa operesheni.

Mott amekanusha kesi ya mauaji, kesi hiyo inaendelea.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment