Bibi Mwenye Miaka 108 Amrudia Mumewe wa Miaka 38

Monday, July 19, 2010 / Posted by ishak /


Bibi wa nchini Malaysia mwenye umri wa miaka 108 amemrudia mumewe mwenye umri wa miaka 38 ambaye alitoka jela hivi karibuni kwa matumizi ya madawa ya kulevya.
Bibi Wook Kundor mwenye umri wa miaka 108 alivuma kwenye vyombo vya habari mwaka 2006 wakati alipofunga ndoa na kijana Muhammad Noor Che Musa ambaye sasa ana umri wa miaka 38.

Wapenzi hao walirudiana siku ya alhamisi baada ya Che Musa kuruhusiwa kutoka kwenye kituo cha kurekebisha tabia ambako alitumikia miezi 12 akipatiwa tiba ya matumizi ya madawa ya kulevya.

"Nimefurahi mume wangu amerudi, nimefurahi tumeonana tena kwakuwa bado nampenda sana", alisema bibi Wook akiliambia gazeti la Utusan Malaysia ambalo liliweka picha yake akimkumbatia mumewe kwenye ukurasa wake wa kwanza.

"Tutarudia maisha yetu ya kawaida kama zamani na nitaendelea kumpa huduma kama wanawake wengine wanavyowahudumia waume zao".

Che Musa alisema kuwa mke wake huyo alimtembelea mara tano alipokuwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia.

Bibi Wook aliripotiwa na vyombo vya habari mwaka jana kuwa yupo tayari kuolewa mara ya 23 na mwanaume mwingine kwa kuhofia Che Musa atakapotoka kwenye kituo cha kurekebisha tabia akiwa ameacha madawa ya kulevya angetafuta mwanamke mwingine wa rika lake.

"Nimemmiss sana, najua nimefanya kosa na nimejutia kosa langu, bado nampenda sana mke wangu", alisema Che Musa.

sorce nifahamishe