Atumia Shada la Maua Kupora Pesa Benki

Thursday, July 22, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja nchini Marekani alitumia njia ya aina yake baada ya kwenda benki akiwa na shada la maua na kulitumia kama silaha kupora pesa.
Mwanaume huyo wa mjini New York nchini Marekani alienda benki akiwa na shada kubwa la maua na kumkabidhi mfanyakazi wa benki kibarua ambacho kilisema kuwa yeye ni jambazi aliyekuja kupora benki.

Polisi waliliambia gazeti la New York Post kuwa wanalifanyia uchunguzi shada la maua ya rangi mbalimbali , njano, nyekundu, kijani na rangi ya machungwa. Maua hayo yaliachwa na jambazi huyo ambaye alifanya uhalifu wake wiki iliyopita.

Kamera za ulinzi zilimuonyesha mtuhumiwa akiwa amesimama mbele na shada lake la maua huku akimkabidhi mfanyakazi wa benki kibarua ambacho aliandika "Nipe pesa zote mia mia na hamsini hamsini, usijaribu kuwa shujaa".

Imeripotiwa kuwa mwanaume huyo aliondoka benki akiwa amechukua kiasi cha dola 440.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment