Inakuwaje Wanigeria Wakazaa Mtoto Mzungu?

Thursday, July 22, 2010 / Posted by ishak /


Wataalamu wa vinasaba (genetic) wanaumiza vichwa kutafuta sababu imekuwaje mama mweusi na baba mweusi wote toka Nigeria wamezaa mtoto wa kizungu mwenye nywele na macho kama ya watoto wa kizungu.
Madaktari nchini Uingereza wanaumiza vichwa kujua sababu ya kuzaliwa kwa mtoto wa kizungu na mama mweusi na baba mweusi ambao wote familia zao mpaka za mababu zao hawajawahi kuchanganya damu na mzungu.

Madaktari wataalamu wamethibitisha mtoto wa kike aliyezaliwa juzi jijini London katika familia ya Benjamin Ihegboro na mkewe Angela ni mzungu na wala si ALBINO.

Mtoto huyo amepewa jina la Kinigeria la Nmachi.

Benjamin na mkewe wote wana asili ya Nigeria na wote wana ngozi nyeusi na wana watoto wengine wawili ambao wote ni weusi.

Angela mwenye umri wa miaka 35 aliliambia gazeti la The Sun la Uingereza kuwa anajivunia mtoto wake huyo ingawa awali alishangazwa sana kuzaa mtoto mzungu kiasi cha kuwauliza madaktari "Huyu ni mtoto wangu kweli?".

"Ni mtoto mrembo -- mtoto wa miujiza", alinukuliwa akisema Angela.

Mtaalamu wa genetics Dr Mark Thomas alisema kuwa kutokana na historia ya familia zao, uwezekano wa Angela na mumewe kuzaa mtoto mzungu ulikuwa ni kati ya moja kati ya mamilioni.

Wataalamu wa genetics nchini Uingereza wanamfanyia uchunguzi mtoto Nmachi ili kujua sababu ya kuzaliwa akiwa na asili ya watu wa ulaya.

Lakini hata hivyo baba yake alisema kuwa hajali sana rangi aliyozaliwa nayo mtoto huyo.

"Ni mtoto mwenye kuvutia na tunampenda", alisema Benjamin na kuongeza "Hata kama angezaliwa akiwa wa njano au wa kijani, tungeendelea kumpenda


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment