Mrembo Mwenye Matiti Makubwa Kuliko Wote Duniani Apigania Maisha Yake

Monday, July 19, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamke mwenye matiti makubwa kuliko wanawake wote duniani ametakiwa achague moja matiti hayo yaondolewe ili aweze kuishi au la afariki akiwa na rekodi yake ya matiti makubwa kuliko wanawake wote duniani.
Sheyla Hershey alipata maambukizi kwenye matiti yake wakati akifanyiwa operesheni ya kuyaongeza matiti yake ambayo yana ukubwa wa 38KKK.

Mrembo huyo wa Brazili mwenye umri wa miaka 30 aliambiwa na madaktari kuwa kuna uwezekano wa asilimia 80 ataweza kuliokoa titi lake moja. Lakini mrembo huyo amesema kuwa ni bora matiti yote yaondolewe kuliko abaki na titi moja.

"Uwezekano wa kuyaokoa matiti yake yote mawili ni mdogo sana kati ya asilimia 10 na 20", alisema Sheyla.

Sheyla alikuwa anafanyiwa operesheni nchini Marekani ili kurekebisha matiti yake ambayo yalipata maambukizi alipofanyiwa operesheni nchini Brazili mwaka jana.

Hiyo ilikuwa operesheni yake ya 10 ya kurekebisha matiti yake tangu alipojifungua mtoto mwaka jana.

Madaktari wa Marekani walikataa kuongeza ukubwa wa matiti yake kwakuwa ni marufuku nchini Marekani kuweka zaidi ya lita 4.5 za silicone kwenye matiti.

Maambukizi aliyopata yalisababisha apate tabu kupumua.

"Niko kwenye maumivu makali ambayo najaribu kuyapunguza kwa kunywa madawa, maambukizi niliyopata ni sawa sawa na kansa", alisema Sheyla.

"Njia pekee ya kuondokana na maumivu haya ni kuyaondoa matiti haya", alisema Sheyla ambaye alikuwa akijivunia sana rekodi yake ya kuwa mwanamke mwenye matiti makubwa kuliko wanawake wote duniani.


source nifahamishe