Fella Ageukia Qaswida

Saturday, July 24, 2010 / Posted by ishak /


MENEJA wa kundi la TMK Wanaume Family, Saidi Fella ameamua kumgeukia mungu na kukisaidia chuo cha Almadrasat Chalama Islamia kutoa albamu yake ya nyimbo za Qaswida.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Fella alisema kuwa ameamua kukisaidia chuo hicho ambacho kiko Mbagala Kizuiani kutoa albamu ikiwa ni harakati ya kutangaza habari za mungu kupitia Qaswida.

"Hiki ni chuo ambacho mimi nilisoma, kwa hiyo nimeona ni vyema nikawasaidia kutoa albamu hii ili waweze kufikisha ujumbe wao kwa jamii kupitia Qaswida," alisema Fella.

Fella alisema kuwa albamu hiyo ambayo tayari imeshaingia sokoni ina nyimbo nne ambazo ni Mazingira uliobeba jina la albamu, Ukimwi na Ndoa.

Alisema kuwa anaamini Qaswida kama zitapewa nafasi zinaweza kufanya vyema katika ulimwengu wa muziki na kusaidia vilivyo kuiweka jamii katika mstari ulionyyoka.

"Qaswida mara nyingi nyimbo zake ni zile ambazo haziipotoshi jamii, na ni muziki ambao wahusika wake wanatakiwa kuweka mbele huduma zaidi za kijamii ukilinganisha na gospo ambao umegeuka kuwa muziki wa kibiashara zaidi," alisema Fella.

source nifahamishe