Afariki Kwasababu ya Imani Yake

Wednesday, May 19, 2010 / Posted by ishak /


Kijana wa kiingereza ambaye ni muumini wa kanisa la mashahidi wa Yehova amefariki dunia baada ya kukataa kuwekewa damu alipopata ajali mbaya ya gari kwakuwa mafundisho ya dini yake yanakataza watu kuwekewa damu za watu wengine.
Joshua McAuley, 15, alikuwa amesimama mbele ya duka moja mjini Smethwick, West Midlands wakati gari lililopoteza muelekeo lilipomgonga yeye na watu wengine wawili kabla ya kutinga ndani ya duka hilo.

Katika ajali hiyo mbaya Joshua alipata majeraha makubwa tumboni na miguuni na alilazimika kuwahishwa hospitali kwa njia ya helikopta kutokana na hali yake kuwa mbaya sana.

Joshua alipoteza damu nyingi sana kwenye ajali hiyo lakini alikuwa akijitambua wakati alipokuwa akiwahishwa hospitali.

Madaktari walipotaka kumwekea damu, Joshua alikataa na kuwaambia madaktari kuwa dini yake inakataza watu kuwekewa damu za watu wengine.

Joshua aliweka wazi kuwa kanisa lake la mashahidi wa Yehova linakataza watu kuwekewa damu za watu wengine.

Joshua aligoma kata kata kuwekewa damu na kwa kuwa sheria haziruhusu madaktari kuwalazimisha wagonjwa vitu wasivyovitaka, madaktari waliacha kumwekea damu.

Masaa sita baada ya ajali hiyo Joshua alipoteza maisha yake.

Familia ya Joshua imeviomba vyombo vya habari vikae mbali wakati wakiombeleza kifo cha mpendwa wao.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment