Hasira za Kufumaniwa na Kuachwa Solemba

Wednesday, May 19, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamke wa nchini Kanada ambaye alikuwa akiisaliti ndoa yake hadi mumewe alipogundua kwa kupitia namba zilizopo kwenye bili ya simu, ameifungulia kesi kampuni yake ya simu kwa kupelekea ukware wake ugundulike na anataka alipwe fidia sawa na Tsh. Milioni 800.
Gabriella Nagy, 35, anaidai fidia kampuni yake ya simu kwa kuingilia masuala yake binafsi na kupelekea aachwe na mumewe.

Gabriella anadai fidia sawa na Tsh. Milioni 800 toka kwa kampuni ya simu ya Rogers Wireless baada ya mumewe kugundua kuwa anaisaliti ndoa yake kupitia namba zilizoandikwa kwenye bili yake ya simu.

Katika madai aliyofungua mahakamani, Gabriela alisema kuwa aliitaka kampuni hiyo ya simu imtumie bili yake ya simu kwa jina lake lakini kampuni hiyo iliijumlisha bili ya simu pamoja na bili ya TV na internet na kuzituma kwa jina la mumewe.

Mumewe alipata shauku ya kujua kulikoni alipoona namba moja imepigwa mara nyingi sana kuliko kawaida, alipoipiga namba hiyo aliambiwa na mwanaume aliyepokea kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Gabriela.

Mumewe aliamua kumuacha Gabriela pamoja na watoto wake na kwenda kuishi sehemu nyingine.


"Kinachoniuma sana ni kwamba uhusiano wenyewe ulikuwa umeisha wakati mume wangu alipogundua" alisema Gabriela na kuongeza kuwa aliiamini kampuni ya simu isingemuangusha na kupelekea kuvunjika kwa ndoa yake.

Katika utetezi wake, kampuni hiyo ya simu ilisema kuwa haiwezi kukubali lawama za kuvunjika kwa ndoa ya Gabriela kwasababu ya bili ya simu waliyoituma.

"Kwa vyovyote vile ndoa yao ingevunjika tu kama mumewe angegundua usaliti wake kwa njia nyingine yoyote ile", ilisema taarifa ya utetezi ya kampuni hiyo.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment