Wazazi wa watoto ombaomba wa mitaani kusakwa

Tuesday, May 18, 2010 / Posted by ishak /

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto imesema ipo katika mikakati ya kuwasaka wazazi wote wanaowatuma watoto wao kwenda kuombaomba barabarani wa lengo la kujipatia pato la siku.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Dk. Lucy Nkya wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya famuilia.


Alisema kwa sasa serikali iko katika mikakati hiyo kabambe ya kuhakikisha inawatafuta wazazi hao ambao wanasababisha kuwe na ongezeko la watoto wa mitaani nchini kote katika ila pembe hasa mijini.

Alisema licha ya serikali kupanga mikakati hiyo ya kuwachukulia hatua wazazi wanaowatuma watoto kuomba mitaani, pia iko katika mipango ya kujua kuna watoto wangapi mitaani ili watoto hao wasaidiwe.

Alisema inafanya sense maalumu ya kujua idadi ya watoto hao ombaomba ili kuwapeleka katika vituo mbalimbali na haiwezi kutekeleza hayo hadi ijue idadi ya watoto hao.

Alisema serikali inajua kuna baadhi ya familia zinakabiliwa na changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na kukosa mahitaji muhimu ya chakula , mavazi, malazi na kupata huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

“ Hivyo tutajaribu kusaidia na serikali haitaweza kusaidia wote ila mkakati uliopo kuwapunguza watoto hao ambao wengine hawana ulazima wa kuwepo mitaani” alsiema


source nifahamishe