Joto la Bangi Lamuua

Tuesday, May 18, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume wa nchini Uingereza aliyekuwa akilima bangi ndani ya nyumba yake amefariki kutokana na joto la taa alizoziweka kusaidia mimea ya bangi kukua haraka.
Luke Holmes mwenye umri wa miaka 28, alikutwa amefariki chumbani kwake kutokana na joto lililotoka kwenye shamba lake la haramu la bangi ndani ya nyumba yake iliyopo Halifax, West Yorks.

Luke alifariki baada ya kuzidiwa na joto kali lililotokana na taa alizoziweka kwenye shamba lake la bangi ili kuifanya mimea ya bangi ikue haraka.

Maiti yake iligundulika siku tatu baada ya kufariki kwake baada ya marafiki zake kuzamia nyumbani kwake kupitia mlango wa nyuma.

Nyumba yake ilikuwa na joto kali sana zaidi ya nyuzi joto 40C.

Polisi walipata tabu kidogo kuingia kwenye nyumba yake ambayo ilikuwa na mahema matatu ya mashamba ya bangi ambayo yalikuwa na taa zenye kutoa joto kali sana.

Polisi wamethibitisha kuwa kifo cha Luke kimetokana na joto kutoka kwenye shamba lake la bangi.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment