Wanaume Wanaowasaidia Wake Zao Kazi za Nyumbani Ndoa Zao Hudumu

Thursday, May 20, 2010 / Posted by ishak /


Wanaume ambao huwasaidia wake zao kazi mbalimbali za nyumbani kama vile kupika, kuosha vyombo na kuwaogesha watoto, ndoa zao hudumu muda mrefu kulinganisha na wale wanaosubiria kufanyiwa kila kitu na wake zao.
Utafiti uliofanywa na watafiti wa chuo cha London School of Economics (LSE) cha Uingereza umeonyesha kuwa wanaume wanaowasaidia wake zao kazi za nyumbani ndoa zao hudumu muda mrefu kulinganisha na wanaume ambao hawependi kuwasaidia kazi za nyumbani wake zao.

Utafiti huo ulisema kuwa ndoa ambazo mke na mume wote wanafanya kazi huwa katika hatari kubwa ya kuvunjika iwapo mume hamsaidii mkewe kazi za nyumbani.

Utafiti huo uliopewa jina la "Men's Unpaid Work and Divorce" ulihusisha familia 3500 za Uingereza.

Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuwa wanaume ambao waliwasaidia wake zao kazi za nyumbani kama vile kwenda sokoni, kuosha vyombo, kupika na kuwaangalia watoto ndoa zao zilionyesha kuwa imara zaidi.

Hata hivyo utafiti huo ulisema kuwa ndoa za watu wa zamani zilidumu sana kwa kuwa mke alikuwa hafanyi kazi akijishughulisha na kazi za nyumbani pekee wakati mume alifanya kazi kutafuta chakula kwaajili ya familia.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment