Amchinja Mkewe Kwa Kunyimwa Unyumba Kwa Miaka 21

Tuesday, March 09, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja wa nchini Ufaransa amemchinja mkewe kwa kutumia kisu kidogo cha jikoni baada ya kukasirishwa na mkewe ambaye aliamua kuitunza bikira yake na kukataa kumpa unyumba kwa miaka 21 ya ndoa yao kwasababu ya alikuwa hataki kupata watoto.
Philippe Cousin mwenye umri wa miaka 53 alimchinja mkewe wa ndoa ya miaka 21 Nicole Cousin mwenye umri wa miaka 47 baada ya Nicole kuendelea kukataa kufanya naye mapenzi kwa kuhofia kupata watoto.

Nicole alikutwa amefariki kwenye nyumba yao katika mji wa Calais kaskazini mwa Ufaransa.

Philippe aliwaambia polisi kuwa mkewe alikataa kufanya naye mapenzi kwa kipindi chote cha ndoa yao akisema kuwa anahofia watoto watakaozaliwa watarithi ugonjwa sugu wa multiple sclerosis (ugonjwa unaosababisha madhara kwenye ubongo na uti wa mgongo) ambao umekua ukimsumbua baba yake Nicole.

Uchunguzi wa maiti ya Nicole ulithibitisha kuwa hadi wakati anafariki Nicole alikuwa kweli ni bikira ingawa alikuwa kwenye ndoa kwa miaka 21.

Siku ya tukio hilo ugomvi ulizuka kati ya Philippe na mkewe ambapo Philippe alichukua kisu na kumwekea mkewe shingoni kabla ya kukikata na kukinyofoa kabisa kichwa chake.

Baada ya tukio hilo Philippe aliwapigia simu polisi na kuwaambia "Samahani kwa kuwasumbua, nimemuua mke wangu".

Phillippe alipandishwa kizimbani jana kwa mauaji hayo aliyoyafanya mwezi aprili mwaka juzi.

Wakili wa Philippe alisema kuwa Philippe alifanya mauaji hayo kutokana na kuchanganyikiwa kimawazo kwa kushindwa kuwa baba.

Philippe ambaye hivi sasa anapatiwa matibabu ya kisaikolojia ndani ya jela huenda akahukumiwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia.

source nifahamishe