Auliwa Kwasababu ya Picha Kwenye Facebook

Sunday, March 07, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mwenye wivu aliyekuwa akiishi nchini Trinidad na Tobago alisafiri umbali mrefu hadi Uingereza na kumuua mpenzi wake baada ya kuona picha yake kwenye Facebook akiwa na mwanaume mwingine.
Paul Bristol, 25, alisafiri toka Trinidad and Tobago hadi Uingereza kumfuata mpenzi wake ambaye alipata mpenzi mwingine baada ya kufika Uingereza.

Paul alifanya safari hiyo kutokana na wivu aliokuwa nao baada ya kuona picha ya mpenzi wake huyo kwenye mtandao wa Facebook akiwa na mwanaume mwingine aliyemtambulisha kama mpenzi wake.

Paul alimuua kwa kumchoma choma na kisu Camille Mathurasingh, 27, ndani ya nyumba aliyokuwa akikaa mashariki mwa jiji la London.

Paul ambaye ni fundi wa vifaa vya umeme, alisafiri kwenda Uingereza ndani ya wiki mbili baada ya kuiona picha hiyo kwenye Facebook.

Paul amepandishwa kizimbani nchini Uingereza na alikanusha mashtaka ya mauaji aliyofunguliwa.

Mahakama iliambiwa kuwa Paul na Camille walikuwa wapenzi kwa miaka mitatu nchini Tobago lakini Camille alivyofika Uingereza alipata mpenzi mwingine na kuamua kuuvunja uhusiano wake na Paul kimya kimya.

"Inavyoonekana mpenzi wake alitaka kuuvunja uhusiano wao kimyakimya bila ya kumwambia kuwa amepata mpenzi mwingine", alisema mwendesha mashtaka wa kesi hiyo.

"Aligundua uhusiano wao baada ya kuziona picha zao kwenye Facebook".

Paul alikamatwa na polisi wakati alipokuwa akikimbia baada ya kufanya mauaji huku akiwa na damu usoni na kwenye nguo zake.

Hukumu ya Paul itatolewa baadae mwezi huu.

source nifahamishe.