Mwanafunzi Mahakamani kwa wizi wa Mil.5

Monday, March 08, 2010 / Posted by ishak /

Mwanafunzi Abdallah Miti [18] wa Shule ya Sekondari ya Ari iliyopo Tabata, amefikishwa katika Mahakama ya Ilala ya jijini Dar es Salaam, kujibu tuhuma za wizi wa kuaminika wa Shilingi milioni 5
Mwanafunzi huyo alisomewa mashtaka mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Joyce Minde wa Mahakama hiyo.

Katuga alidai, mtuhumiwa alitenda kosa hilo, Februari 20, mwaka huu katika mtaa wa Garden Ilala jijini Dar es Salaam.

Katuga alidai mwanafunzi huyo aliiba fedha hizo kutoka katika gari namba T 630 aina ya Toyota mali ya Anselem Sigela.
Mtuhumiwa alikana kuhusika na wizi huo na alirudishw rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana aliyopewa.

Ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika wendye uwezo wa kusaini shilingi milioni 5 mahakamani hapo.

Hivyo kesi hiyo iliahirishwa, itatajwa tena Machi 16, mwaka huu.

source nifahamishe