Polisi Anapozimeza Pesa za Hongo Alizopokea

Thursday, March 11, 2010 / Posted by ishak /


Polisi mmoja wa nchini Urusi ametiwa mbaroni kwa kupokea rushwa na kisha kujaribu kuzimeza noti za pesa alizopokea ili kupoteza ushahidi.
Polisi mmoja wa nchini Urusi ameingia matatani kwa kupokea rushwa ya pesa za Kirusi ruble 2000 sawa na Tsh. 95,000 na kisha kujaribu kuzimeza noti za hongo hiyo ili kupoteza ushahidi.

Afisa wa polisi, Alexei Nikolayev, alichukua rushwa toka kwa dereva aliyemkata kwa makosa ya barabani ili asimchukulie hatua dereva huyo.

Lakini dereva wa gari hilo aliwapa taarifa polisi ambao walimkamata afisa huyo wa polisi wakati akipokea rushwa.

Ili kupoteza ushahidi afisa huyo wa polisi alijifungia kwenye gari la polisi na kuanza kuzitafuna noti za pesa hizo.

Afisa huyo anaendelea kuchunguzwa na atafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika.

source nifahamishe