Makahaba 40,000 Kwenda Afrika Kusini Wakati wa Kombe la Dunia

Monday, March 08, 2010 / Posted by ishak /


Makahaba wapatao 40,000 toka nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kuingia nchini Afrika Kusini wakati wa kombe la dunia litakalofanyika nchini humo baadae mwaka huu.
Wanawake wapatao 40,000 wanatarajiwa kuingia nchini Afrika Kusini kufanya kazi ya ukahaba wakati wa mwezi mmoja wa kombe la dunia ambalo litafanyika baadae mwaka huu nchini humo.

Afrika Kusini inaongeza ulinzi kwenye mipaka yake ili kuzuia wimbi hilo la makahaba ambao wengi wao wanatarajiwa kutoka nchi za ulaya mashariki.

Zaidi ya watu 450,000 toka nchi mbali mbali duniani wanatarajiwa kuingia nchini Afrika Kusini kwaajili ya kombe la dunia.

Akiongea katika kikao na umoja wa mataifa kuhusiana na vita dhidi ya madawa ya kulevya na uhalifu nchini humo, David Bayever, ambaye ni makamu mwenyekiti wa mamlaka ya kupambana na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini alisema kuwa maafisa wa Afrika Kusini wanahofia wimbi kubwa la wanawake wanaotarajiwa kuingia nchini humo kwaajili ya biashara ya ukahaba.

"Tumepewa taarifa na waandaaji wa kombe la dunia kuwa wamepata taarifa kuwa wanawake 40,000 wameajiriwa kuja kufanya ukahaba wakati wa kombe la dunia", alisema.

"Hali inatisha sana kutokana na kwamba asilimia 16 ya idadi ya watu wana maambukizi ya virusi vya ukimwi", alisema.

Bayever alisema kuwa wamehakikishiwa na idara ya uhamiaji kuwa ulinzi utaongezwa kwenye mipaka na ukaguzi wa pasport utaimarishwa.

source nifahamishe