Mwanamke Apata Ajali Akijionyoa Nywele za Sehemu za Siri

Thursday, March 11, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamke mmoja wa nchini Marekani huenda akatupwa jela baada ya kuligonga gari jingine alipoamua kuzinyoa nywele zake za sehemu za siri huku akiendesha gari.
Megan Mariah Barnes mwenye umri wa miaka 37 aliamua akiendesha gari kuelekea kwa mpenzu wake kusini mwa Florida, Marekani wakati ajali hiyo ilipotokea, televisheni ta WFOR-TV imeripoti.

Megan aliamua kujiweka sawa kabla hajafika kwa mpenzi wake na kuanza kuzinyoa nywele za sehemu zake za siri huku akiendesha gari huku akiamuachia mumewe wa zamani aliyekuwa kwenye gari hilo awe anabadilisha muelekeo wa usukani.

"Kama nisingekuwepo kwenye eneo la tukio nisingeliamini tukio hili", alisema afisa wa polisi Gary Dunick.

Megan alijitetea kuwa aliamua kujionyoa nywele zake za siri huku akiendesha gari ili awe tayari tayari atakapofika kwa mpenzi wake.

Megan aliligonga lori gari lililokuwa mbele yake wakati huo akiwa kwenye spidi ya kilomita 72 kwa saa.

Siku moja kabla ya tukio hilo, Megan alinyang'anywa leseni yake baada ya kufungiwa kuendesha gari miaka mitano kutokana na makosa ya kuendesha gari huku akiwa amelewa.

Megan huenda akahukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kuendesha gari kizembe, kuendesha gari bila ya leseni, kuendesha gari bila ya bima na kuondoka kwenye eneo la ajali huku akiwa na majeraha.

source nifahamishe