Katuni Nyingine ya Kumkashifu Mtume Yachapishwa Sweden

Thursday, March 11, 2010 / Posted by ishak /


Mgazeti mengi ya Sweden jana jumatano yaliichapisha katuni nyingine ya kumkashifu mtume Muhammad (S.A.W) katika kuonyesha upinzani wao kwa jaribio la kumuua mchora katuni wa Sweden aliyemchora mtume akiwa na umbile la mbwa.
Mgazeti makubwa ya Sweden jana jumatano yalichapisha katuni ya kumkashifu mtume Muhammad (s.a.w) ambayo ilisababisha waislamu saba wale njama za kumuua mchora katuni aliyeichora katuni hiyo.

Kichwa cha mchora katuni wa Sweden Lars Vilks kimewekewa zawadi ya dola 100,000 na Al-Qaeda kama zawadi kwa mtu atakayemuua mchora katuni huyo.

Waislamu saba walikamatwa juzi nchini Ireland wakidaiwa kula njama za kumuua Vilks ambaye alichora katuni ya mtume akiwa na umbile la mbwa.

Gazeti la Dagens Nyheter la nchini Sweden liliichapisha katuni hiyo iliyosababisha mtafaruku huku ikisema kuwa Lars Vilks hayupo peke yake kwenye mgogoro huu.

"Vitisho vyovyote vya maisha yake kwa upande mmoja ni sawa na kuwatishia maisha raia wote wa Sweden", lilisema gazeti hilo katika sehemu yake ya maoni ya mhariri.

Gazeti liliendelea kwa kuitaka serikali ya Sweden impe Vilks ulinzi wowote unaohitajika.

"Mamlaka husika lazima zichukue hatua dhidi ya shambulio linalotaka kuharibu haki yetu ya msingi ya uhuru wa kujieleza", lilisema gazeti hilo.

Gazeti jingine la Expressen nalo liliichapisha katuni hiyo likisisitiza kuwa ni muhimu kulinda uhuru wa kujieleza ambao unatishiwa amani.

"Jamii lazima ionyeshe kuwa haitatishika na vitisho na kuwa tayari kupigania uhuru wa kujieleza", lilisema gazeti hilo.

Vilks akiongea kuhusiana na jaribio la kumuua alisema kuwa hajatishika na kukamatwa kwa watu saba nchini Ireland waliotaka kumuua.

Vilks aliiambia televisheni ya TV4 kuwa angerudia tena kuichora katuni hiyo iwapo atapata nafasi tena.

Vitisho vya kumuua Vilks vimekwenda sambamba na majaribio kadhaa ya kumuua mchora katuni wa Denmark Kurt Westergaard ambaye mwaka 2005 alichora katuni ya mtume akiwa na bomu kwenye kichwa chake.

"Vitisho dhidi ya Vilks vinasikitisha", alisema Westergaard akiliambia gazeti la Expressen na kuongeza "Nimefurahishwa na ushujaa wake na jinsi alivyoweza kuhimili vitisho".

source nifahamishe

1 comments:

Anonymous on August 4, 2010 at 10:53 PM

HOW DOES SODOMY AND MARRIAGE OF SAME SEX RELATE WITH REFERENCE TO BIBLE, YOU HAVE A LOT TO PUBLISH THAT CONCERNS YOURSELF.

Post a Comment