Mtoto wa Miaka 3 Ajiua Kwa Kujipiga Risasi

Thursday, March 11, 2010 / Posted by ishak /


Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu wa nchini Marekani amefariki dunia baada ya kujipiga risasi ya tumbo wakati alipokuwa akichezea bastola ya kweli ya baba yake akidhania anachezea bastola feki inayotumika kwenye deki ya gemu ya Nintendo Wii.
Mtoto Cheyenne Alexis McKeehan mwenye umri wa miaka mitatu alijipiga risasi ya tumbo kwa kutumia bastola ya baba wake wa kambo aliyoikuta kwenye meza sebuleni.

Mtoto huyo alichukua bastola hiyo ya kweli na kuanza kuichezea akidhani anachezea bastola feki inayotumika kwenye gemu ya Nintendo Wii.

Mama wa mtoto huyo alikuwa amekaa hatua chache na mtoto huyo akitumia kompyuta huku mtoto wake mwingine mwenye umri wa miezi mitatu alikuwa amelala chini kwenye sakafu.

Wachunguzi wa kesi hiyo wamesema kuwa bila shaka mtoto huyo alishindwa kutofautisha bastola ya kweli na bastola feki ya Nintendo Wii.

Mama wa binti huyo, Tina Ann Cronberger mwenye umri wa miaka 32, alisema kuwa binti yake alikuwa mara kwa mara akiitumia bunduki feki kwenye kucheza gemu za Nintendo Wii.

Tukio hilo lilitokea jumapili jioni kwenye kitongoji cha Wilson, Tennesee nchini Marekani wakati baba wa kambo wa mtoto huyo, Douglas Cronberger, 32, alipochukua bunduki yake na kutoka nje alipohisi kuna mwizi ameingia nyumbani kwake.

Baada ya kuizunguka nyumba yake bila ya kumuona mwizi yoyote, alirudi ndani na kuiweka bastola kwenye meza sebuleni na kisha kwenda kulala.

Muda mfupi baadae, Chayenne alijipiga risasi na alipowahishwa hospitalini alifariki njiani.

Haijajulikana kama wazazi wa mtoto huyo watafunguliwa mashtaka au la.

source nifahamishe