Mapenzi Yasababisha Atupwe Jela

Thursday, March 11, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja wa nchini Ujerumani ambaye alitaka kumstaajabisha mpenzi wake kwa kuruka ukuta kuingia nyumbani kwake usiku akiwa amebeba zawadi ya ua la waridi na mvinyo amejikuta akienda jela baada ya mpenzi wake kuita polisi akidhania ameingiliwa na wezi,
Mwanamke mmoja wa nchini Ujerumani huku na hofu kubwa ya maisha yake aliwaita polisi baada ya kuhisi kuna mwizi amevamia nyumbani kwake usiku kwa kuruka ukuta.

Polisi walishangazwa kumuona mwanaume waliyemkamata aliyehisiwa kuwa ni mwizi alikuwa ni mpenzi wa mwanamke huyo akiwa amebeba ua la waridi na mvinyo. Hata hivyo polisi waliamua kumtia mbaroni mwanaume huyo.

"Alikuwa akijaribu kumfanyia suprise mpenzi wake kwa kumpelekea ua na mvinyo saa sita usiku lakini mpango wake ulienda vibaya", alisema msemaji wa polisi.

Polisi walisema kuwa mwanaume huyo alijaribu kukimbia baada ya kuwaona polisi lakini hakufanikiwa kutoroka na alitiwa mbaroni wakati huo huo.

Mwanaume huyo aliamua kuwagaia polisi chupa yake ya mvinyo kama shukurani yake kwa polisi waliomkamata kwa kumchukulia kama rafiki yao na kutompa misukosuko.

source nifahamishe