Ruhsa Kujiua Ukitimiza Miaka 70

Thursday, March 11, 2010 / Posted by ishak /


Serikali ya Uholanzi inategemea kupitisha sheria yenye utata itakayowaruhusu watu wenye umri kuanzia miaka 70 kujiua wenyewe kwa msaada wa madaktari iwapo watahisi kuwa wametosheka na maisha duniani.
Watu wenye umri zaidi ya miaka 70 wataruhusiwa kujiua kwa kusaidiwa na madaktari iwapo wataona wameishatosheka na maisha yao hapa duniani.

Watu ambao hawana ujuzi wa udaktari watapewa mafunzo jinsi ya kuwasaidia wazee wenye umri zaidi ya miaka 70 kujiua kwa kutumia sindano za simu hospitalini.

Bunge la Uholanzi linatarajia kuujadili muswada wa sheria hiyo baada ya watu wanaoipigia kampeni sheria hiyo kukusanya sahihi za watu 112,500 wanaounga mkono sheria ya kuruhusu watu kujiua.

Watetezi wa sheria hiyo wamesema kuwa kupitishwa kwa sheria hiyo kutawawezesha wazee kuamua kufariki kimya kimya kwa utulivu pindi watakapoona wamechoka kuishi na wanataka kuepukana na pilikapilika za dunia.

Wasaidizi wa madaktari watakaokuwa wakichanganya dawa ya sumu itakayotumika kuwaulia wazee watakaojitokeza.

Hata hivyo mashirika ya kidini yameelezea kupinga kwake kuruhusu watu kujiua eti kwasaabu ya kuyachoka maisha.

source nifahamishe