Daktari Anayetumia Limao Kusafishia Vidonda Aua Watu Saba

Wednesday, January 20, 2010 / Posted by ishak /


Daktari wa Ujerumani ambaye alikuwa akitumia maji ya limao kusafishia majeraha ya operesheni amefunguliwa mashtaka baada ya kupelekea vifo vya watu saba.
Dokta Arnold Pier amehukumiwa kifungo cha nje cha miezi 15 baada ya njia yake ya kusafisha majeraha kwa kutumia maji ya limao kusababisha vifo vya watu saba.

Kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani la Bild, katika kubana matumizi katika zahanati yake Dr. Pier badala ya kutumia madawa ya kusafishia vidonda na majeraha alikuwa akitumia maji ya malimao kusafishia vidonda.

Mwanamke mmoja alifariki baada ya kupata maambukizi baada ya majeraha yake baada ya operesheni kusafishwa kwa kutumia maji ya limao.

Dr Pier ambaye ni mmiliki wa zahanati ambayo vifo hivyo vilitokea, anatuhumiwa pia kuwafanyia wagonjwa operesheni zisizo za lazima ili kujiingizia pesa zaidi.

Hospitali ya Dr. Pier ilikuwa katika hali ngumu ya kiuchumi wakati Dr. Pier alipobuni mbinu za kubana matumizi ikiwemo njia ya kutumia majji ya malimao kusafishia majeraha.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo, Jaji Lothar Beckers alisema kuwa njia ya kutumia maji ya malimao mbali ya kuwasababishia maambukizi wagonjwa iliwasababishia maumivu makali zaidi.

Dr Pier pamoja na madaktari wenzake watatu wamefunguliwa mashtaka 64 ya kudhuru mwili kuhusiana na wagonjwa 18.


source nifahamishe