Hali ilivyo Nchini Haiti ni Mfano wa Jahanamu

Sunday, January 17, 2010 / Posted by ishak /


Hali iliyopo nchini Haiti baada ya tetemeko kubwa la ardhi inatisha sana hakuna tena utawala wa sheria mwenye nguvu anamuonea mnyonge ili apate chochote cha kukaganga njaa, maiti zimezagaa kila kona kiasi cha kwamba zinatumiwa kama vizuizi vya barabarani.
Jinsi siku zinavyozidi kwenda mbele mamia ya watu wanazidi kufariki kutokana na njaa na maradhi mbali mbali huku maelfu ya watu wakiwa wamezikwa hai chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea nchini Haiti.

Tetemeko hilo la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 limeuharibu kwa asilimia 90 mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.

Majengo mengi sana likiwemo jengo la ikulu na jengo la Umoja wa mataifa nchini Haiti yameporomoka na kuwafukia maelfu ya watu.

Hadi sasa jumla ya watu 50,000 wameishatibitishwa kufariki na idadi kamili ya watu waliofariki inakisiwa kuwa zaidi ya watu 200,000.

Maiti zimezagaa kila kona kiasi cha kwamba watu ambao walishindwa kupata msaada ulioletwa na mataifa ya nje waliamua kuzikusanya maiti na kuzijaza barabarani kuonyesha hasira zao.

Wezi nao wameongezeka kila kona, mwizi mmoja ambaye alikamatwa akimuibia mmoja wa wahanga wa tetemeko hilo la ardhi aliuliwa na kisha maiti yake kuburuzwa barabarani kabla ya kuchomwa moto.

Kwa hali iliyopo sasa nchini Haiti, kila mtu anajiangalia mwenyewe. Watu wenye nguvu wamekuwa wakitumia silaha zao kama vile visu na silaha nyinginezo kuwatishia watu wengine ili waweze kuwanyang'anya mali zao.

Misaada toka mataifa mbali mbali duniani imesaidia kuokoa maisha ya baadhi ya watu lakini bado haitoshi na haijawafikia watu wengi kutokana na kuharibika kwa njia zote za mawasiliano.

Hospitali zote zimefurika wagonjwa na maiti zimezagaa pia kila kona kiasi cha kwamba zimekuwa zikikusanywa na kulundikwa pamoja maiti za wanyama vile.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment