Mtoto wa Miaka 11 Aruhusiwa Kuendesha Gari, Aitekeza Familia Yake

Sunday, January 17, 2010 / Posted by ishak /


Mtoto mwenye umri wa miaka 11 wa nchini Marekani ambaye aliruhusiwa kuendesha gari na wazazi wake, alisababisha ajali iliyosababisha kifo chake, mama yake na dada yake.
Polisi nchini Marekani wanafanya uchunguzi kujua ni kwanini mtoto wa kiume Jose Manuel Silva Covarrubias mwenye umri wa miaka 11 aliruhisiwa kuendesha gari lililopata ajali baada ya dereva hiyo mtoto kushindwa kusimama kwenye mataa.

Gari lililokuwa likiendeswa na mtoto Jose likiwa limembeba mama yake, dada yake na mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 34 liligongwa na gari jingine aina ya Ford baada ya kukatiza kwenye mataa huku taa nyekundu zikiwa zimewaka.

Polisi wanachunguza ilikuwaje Jose aliruhusiwa kuendesha gari aina ya Honda na kupelekea kutokea kwa ajali hiyo katika kitongoji cha Porterville, California.

Polisi wanatarajia kumhoji mtu pekee aliyenusurika katika ajali hiyo rafiki wa familia hiyo, Froylon Gonzalez mwenye umri wa miaka 34 aliyekuwa amekaa siti ya pembeni ya dereva huyo mtoto.

Gonzalez alinusurika kwakuwa alikuwa amevaa mkanda wakati mama wa mtoto huyo Maria Covarrubias, 30 na dada wa mtoto huyo Elizabeth Silva Covarrubias,6, walifariki baada ya kurushwa toka siti za nyuma kwakuwa hawakuwa wamevaa mkanda.

Kaka wa majeruhi aliyenusurika maisha yake alisema kuwa familia hiyo ilikuwa ikitoka kwenye mazoezi ya soka ya Jose na pia alisema kuwa hakuwahi kumuona Jose akiendesha gari kabla ya siku ya ajali hiyo.

source.nifahamishe

0 comments:

Post a Comment