Kiongozi wa umoja wa vijana wa chama tawala nchini Zambia ametishia kuwa vijana wa chama hicho watambaka 'mande' mwanasiasa mwanamke anayeonyesha upinzani wa sera za rais wa Zambia.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama tawala nchini Zambia cha MMD bwana Chris Chalwe ametishia kumbaka mwanansiasa mwanamke Bi. Edith Nawakwi ambaye amekuwa akiukosoa sana uongozi wa rais Rupiah Banda.
"Tutambaka mande (mtungo) Nawakwi iwapo ataendelea kumshambulia rais", alisema Chalwe kuuambia umati wawati uliokusanyika kwenye mkutano wa kisiasa.
Chalwe alitoa kitisho hicho katika kumlinda rais Banda ambaye anajiandaa na uchaguzi mkuu mapema mwaka ujao.
Nawakwi ambaye ni kiongozi wa FDD alimuunga mkono Banda wakati wa uchaguzi mwaka 2008 lakini sasa amekuwa akimkosoa kuwa uongozi wake umefeli.
"Rais amechaguliwa na watu wa Zambia hivyo anastahili heshima toka kwa wananchi wote na mtu yoyote atakeyemkosoa tutambaka mande", aliongeza Chalwe.
Chalwe anajulikana kwa ukorofi wake na hivi sasa anakabiliwa na kesi mahakamani ya kumpiga mwandishi wa habari aliyekuwa akiripoti rais Banda kurudi nyumbani toka Uganda alipofanya ziara mwezi julai mwaka jana.
Akiongelea tukio hilo la kutishiwa kubakwa, bi Nawakwi alisema kuwa jambo lolote litakalomtokea basi rais Banda ndiye atakayekuwa wa kulaumiwa.
Bi Nawakwi aliongeza kuwa amewasiliana na wanasheria wake kuhusiana na tishio hilo ambalo alisema halitoki kwa Chalwe pekee bali linatoka kwa serikali ya rais Banda kwa kuwa Chalwe na vijana wa MMD wanapata sapoti toka serikalini.
source nifahamishe
Mwanasiasa Zambia Atishia Kumbaka 'Mande' Mpinzani wa Rais
Wednesday, January 20, 2010
/
Posted by
ishak
/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment