MBWA MZEE ZAIDI DUNIANI AFARIKI

Sunday, January 17, 2010 / Posted by ishak /


Mbwa huyo aliyekuwa akiitwa Otto, na aliyekuwa na umri wa miaka 20 alikufa siku ya ijumaa, mwili wake utachomwa na majivu yake kuzikwa.

Mmiliki wa mbwa huyo, mwanamke Lynn Jones, 54, kutoka Shrewsbury, Shropshire, Uingereza, alisema: "Nililia siku nzima tangu asubuhi. Kwangu hili ni balaa kubwa.

"Alikufa saa nne na dakika kumi asubuhi siku ya ijumaa. Hapa nilipo naona kama nimepoteza mkono wangu wa kulia. Kwangu alikuwa kama mtoto wangu wa kiume.



“Ninafurahi tu kwamba hateseki tena na maumivu, lakini nilitaka kuwa naye milele.”
Bi Jones na mumewe Peter, 68, walimpeleka Otto kwenye kituo cha tiba za wanyama ili akauawe baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi.

"Tuligundua alikuwa na uvimbe mkubwa tumboni. Hakuweza kukaa au kulala kwa raha. Hivyo tulimpeleka kwa madaktari wa wanyama akauawe ili kuyamaliza mateso yake,” alisema Jones.

Otto, ambaye angekuwa na umri wa miaka 21 tarehe 14 Februari mwaka huu, ndiye mbwa mzee zaidi aliyetajwa katika kitabu cha Guinness Book of Records mwezi Oktoba mwaka jana.


source.globulpublisher

0 comments:

Post a Comment