Mashirika ya ndege ya KLM na Air France yataanza kuwalipisha nauli za watu wawili, watu wanene ambao wanashindwa kujibana kwenye siti moja.
Watu wanene ambao hawaenei kwenye siti moja ya kwenye ndege watalazimika kulipa nauli za watu wawili iwapo watasafiri kwenye ndege za KLM na Air France.
Msemaji wa mashirika hayo, Monique Matze, alisema kuwa watu wanene sana ambao hawatoshi kwenye siti moja watalazimika kulipia asilimia 75 ya nauli ya siti ya pili.
Matze alisema kuwa uamuzi huo unatokana na sababu za kiusalama.
"Inatubidi tuhakikishe kuwa mtu anaweza kujisogeza vizuri na abiria wote wanafunga mkanda ipasavyo kwenye ndege", alisema Matze.
Watu ambao hawaenei kwenye siti moja watalazimika kufunga mkanda kwa kuunganisha mikanda ya siti mbili.
Watu wanene wasiotosha kwenye siti moja watahakikishiwa kutengewa siti mbili watakazotakiwa kuzilipia wakati wa kununua tiketi.
Sheria hiyo mpya itaanza kutumika kuanzia februari moja mwaka huu.
Kiti cha ndege kawaida huwa na unene wa sentimeta 43 na kwa ndege za masafa marefu huwa na unene wa sentimeta 44.
source nifahamishe
Vibonge Kuanza Kulipishwa Nauli za Watu Wawili Kwenye Ndege
Wednesday, January 20, 2010
/
Posted by
ishak
/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment