SENEGAL YAWAKARIBISHA WATU WA HAITI

Sunday, January 17, 2010 / Posted by ishak /


Rais Abdoulaye Wade alisema watu wa Haiti ni wana wa Afrika kwani Haiti ilianzishwa na watumwa waliochukuliwa kutoka Afrika na baadhi wakiaminika kutoka Senegal.

“Rais anatoa fursa hiyo kwa watu wa Haiti watakaokubali kwa hiari yao kurejea katika shina lao,” alisema msemaji wa rais, Mamadou Bemba Ndiaye.

Jumanne iliyopita makumi ya maelfu ya watu waliuawa na wengine kukosa makazi baada ya nchi hiyo kukumbwa na tetemeko la ardhi.

Majengo yameteketea na utoaji wa misaada unakwenda taratibu mno huku watu wakiondoka katika mji mkuu wa nchi hiyo, Port-au-Prince, ambao umeharibiwa vibaya.

“Senegal iko tayari kuwapatia ardhi na hata maeneo makubwa zaidi. Hii itategemea ni watu wangapi wa Haiti watakaoamua kuja,” alisema Ndiaye.

source.globalpublish

0 comments:

Post a Comment