Mwizi wa Simu Akatwa Mkono Somalia

Saturday, January 23, 2010 / Posted by ishak /


Wanamgambo wa kundi la Al Shabab la nchini Somalia wamemkata mkono wa kulia mwanaume aliyekamatwa akiiba simu.
Wanamgambo wa kundi la Al Shabab la nchini Somalia wameukata kwa kutumia jambia mkono wa kulia wa mwanaume mwenye umri wa miaka 30 aliyekamatwa akiiba simu.

Yusuf Sheikh Ahmed alikamatwa akiiba simu kwenye mji wa Merka ambao unatawaliwa na kundi la Al Shabab.

Yusuf alikamatwa mkono wake wa kulia mbele ya mamia ya watu waliokusanyika kushuhudia adhabu hiyo.

"Adhabu hii ni mojawapo ya juhudi zetu za kutokomeza uhalifu kwa sharia za kiislamu, mtu yoyote atakayeiba atakatwa mkono wake", alisema Sheikh Isa Mohamed, ambaye ni mmoja wa maafisa wa Al Shabab.

Jaji wa mahakama ya kiislamu ya mji huo aliamuru Yusuf akatwe mkono wake wa kulia baada ya Yusuf mwenyewe kukiri kosa lake la kuiba simu.

Yusuf aliwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi baada ya kukatwa mkono wake.

Wakati huo huo wanaume wengine ambao walikamatwa wakiwa wamelewa pombe na madawa ya kulevya walicharazwa bakora kati ya 40 na 80.

Kundi la Al Shabab linashikilia maeneo ya kusini na katikati mwa Somalia.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment