MWanajeshi aua mkewe na kisha mwenyewe kujinyonga

Wednesday, January 20, 2010 / Posted by ishak /

ASKARI mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kepteni Deogratius Chache (60), amuua mkewe kwa kumkata kichwa na kisha na yeye kujinyonga hadi kufa huko Tarime Mkoani Mara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime, Costastino Masawe, amesema tukio hilo lilitokea Januari 16 mwaka huu, saa 2 usiku, katika kijiji cha Kiterere Mara.

Alisema askari huyo ambaye ni ofisa mstaafu wa JWTZ alimkata mkewe Aloidia Kambunga [47] na panga sehemu za kichwani na kisha na kuutenganisha mguu wake wakulia kulia na kupatikana kifo hca mma huyo.

Kamanda Masawe alisema kuwa baada ya ofisa kufanya kitendo hicho alitoka eneo la nyumbani kwake kama mita 20 kisha na yeye kwenda kujinyonga kwenye mti kutokana na hasira alizokuwa nazo.

Kamanda Masawe aliviambia vyombo vya habari kuwa, kabla ya tukio hilo kutokea marehemu hao walikuwa na ugomvi siku nyingi kati ya wana ndoa uliopelekea kila mmoja kulala katika chumba chake.

Alisema kuwa ofisa huyo alikuwa akimkanya mkewe ambaye alikuwa ni muuguzi katika Hospitali ya Kitega kuhusiana na tabia ya kutoka nje ya ndoa lakini aliona hakuna maeleweno na baadae waliamua wajitenge vyumba.

Aliongeza kuwa chanzo cha mauaji hayo yalisemekana ni kutokana na wivu wa kimapenzi

Katika tukio la lingine la mauaji mwanaume mmoja anashikiliwa na polisi wilayani Bunda kwa tuhuma za kumpiga mkewe na kumsababishia kifo.

Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Robert Boaz, alisema mtuhumiwa huyo ni Chacha Magoki, mkazi wa Kijiji cha Kihumbu wilayani Bunda.

Kamanda Boaz alisema mwanaume huyo alitiwa mbaroni juzi asubuhi akiwa anasafirisha mwili wa marehemu huyo kutoka hospitalini ili ukazikwe katika kijiji cha Kihumbu.

Ilidaiwa kuwa mwanaume huyo alimpiga mke wake Ester Werema kutokana na kukasirishwa na kitendo cha mke wake kumpa chakula shemeji yake.

Ilidaiwa mume wake kutokana na wivu wa kimapenzi alikuwa akimkanya kitendo cha kuwa karibu na shemeji yake huyo na alikuwa akimpiga mara kwa mara.
Polisi wamesema mwanaume huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote kujibu mashitaka ya mauaji.


sourrce nifahamishe

0 comments:

Post a Comment