Picha Hii ya Michelle Obama Yamponza!

Saturday, January 23, 2010 / Posted by ishak /


Msanii wa Marekani aliyeiweka picha hii ya mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter imembidi aombe ulinzi toka FBI baada ya mamia ya watu kumtumia vitisho vya kumuua.
Scott Baio msanii wa Marekani aliyetamba kwenye series za komedi za Happy Days na Charles in Charge ametumiwa vitisho kibao vya maisha yake baada ya kuweka picha mbaya ya mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Baio aliiweka picha hii ya Michelle Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter ikiwa na maneno "Wow, Obama anaamshwa namna hii kila siku asubuhi".

Picha hii pamoja na maelezo yake ilichukuliwa na watumiaji wengine wa Twitter kama ubaguzi wa rangi.

Haukupita muda mrefu Baio alianza kuandikiwa maoni kwenye ukurasa wake wa Twitter akiambiwa kuwa ni mbaguzi wa rangi na ameweka picha hiyo kumdhalilisha bi Michelle Obama.

Baio alitumiwa vitisho vingi vya maisha yake kiasi cha kumfanya aripoti vitisho hivyo FBI.

"Ni rahisi kuijua nyumba yako Baio na kukumaliza", Mtoa maoni mmoja aliandika huku mwingine akitishia kumdhuru Baio, Mkewe na mtoto wake.

Hata hivyo Baio aliendelea kusisitiza kuwa alikuwa na nia ya kufanya masihara na sio kama ambavyo watu wengine walivyoichukulia picha na maandishi aliyoyaweka.

Baio aliandika pia kwenye ukurasa wake baadhi ya vitisho vya maisha yake alivyotumiwa.

Katika kuonyesha kwamba yeye sio mbaguzi wa rangi Baio aliweka picha yake akiwa pamoja na mwanamke mweusi ambaye ni rafiki wa mke wake.

"Mimi sio mbaguzi wa rangi kwa kuweka picha ya Michelle Obama, rafiki mkubwa wa mke wangu ni Mmarekani mweusi", alisema Baio.

Baio aliandika ujumbe pia kwenye Twitter akiwafahamisha watu kuwa ameisharipoti vitisho alivyotumiwa FBI.

source nifahamishe