Aibu Yamkumba Mkaguzi wa Silaha wa Umoja wa Mataifa

Sunday, January 17, 2010 / Posted by ishak /


Mkaguzi wa silaha wa zamani wa Umoja wa Mataifa aliyepewa madaraka wakati huo kuzikagua silaha za aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein amekumbwa na fedheha kubwa ya ngono za watoto ambapo alijipigisha punyeto mbele ya msichana wa miaka 15 na huenda akatupwa jela miaka saba.
Mpelelezi Scott Ritter mwenye umri wa miaka 48 ambaye alikuwa mkaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq kabla ya kujiuzulu mwaka 1998, anakabiliwa na mashtaka ya ngono za watoto baada ya kunaswa akimtongoza msichana mwenye umri wa miaka 15.

Ritter ambaye anaishi na mkewe, bila kufahamu kuwa alikuwa akichunguzwa kuhusiana na ngono za watoto, alikuwa akiwasiliana kwa njia ya internet na msichana aliyejitambulisha kwa jina la Emily mwenye umri wa miaka 15.

Ukweli ni kwamba Emily hakuwa msichana mwenye umri wa miaka 15 bali ni afisa wa polisi Ryan Venneman aliyekuwa akimchunguza Ritter kuhusiana na ngono za watoto kwenye internet.

Ritter alianza kumwagia sera zake Emily kuanzia mwezi februari mwaka jana akitaka kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Katika kipindi cha miezi tisa bila kufahamu kuwa anachunguzwa, Ritter aliendea kumwaga sera zake na kuna wakati alidiriki hata kujipigisha punyeto live huku akijionyesha kwa kutumia webcam.

Jina la Ritter lilisikika sana wakati wa utawala wa rais George Bush alipotakiwa kukagua silaha za sumu nchini Iraq ambazo mpaka Saddam Hussein ananyongwa mwaka 2006 zilikuwa bado hazijapatikana.

Ritter alishawahi kuingia matatani kwa kosa kama hili la kujihusisha na ngono za watoto mwaka 2001 lakini kesi yake ilifutwa baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha.

Safari hii maafisa wa polisi wamesema kuwa wana ushahidi wa meseji za simu na webcam kumtia hatiani Ritter.

Ritter amefunguliwa kesi mjini Pennsylvania na kesi yake itaanza kusikilizwa mwezi machi. Iwapo atapatikana na hatia anaweza kutupwa jela miaka saba.

source.nifahamishe