Always bandia zakamatwa Arusha

Tuesday, January 26, 2010 / Posted by ishak /

JESHI la Polisi mkoani Arusha limekamata shehena ya taulo bandia za wanawake ‘Always’ zenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 200 ambazo hazifai kwa matumizi hayo.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Bw. Basilo Matei, alisema kuwa shehena hiyo ilikamatwa juzi nyumbani kwa mfanyabiashara maarufu mmoja aishio maeneo la Baraa.

Matei alisema mfanyabiashara huyo kwa sasa jina linahifadhiwa kwa sababu za kipolisi na kusema shehena hiyo ilikuwa na maboksi zaidi ya 10,000 na zinadhaniwa kuingizwa nchini kutoka nchini China na zilishasambazwa katika maeneo ya biashara kinyemela.

Matei alieleza kuwa polisi walifanikiwa kukamata Always hizo bandia baada ya kupata taarifa kutoka kwa kampuni ya Procter & Gambo Ltd ya jijini Dar es Salaam ambayo ni wakala aliyeruhusiwa kuingiza bidhaa hizo nchini.

Alisema kampuni hiyo iligundua bidhaa hizo feki kujaa sokoni kaika maeneo mengi .

Alisema bidhaa hizo zilithibitishwa kuwa ni feki baada ya kutafutwa wataalamu wa mambo ya afya ambao walibainisha kuwa bidhaa hiyo ilikuwa ni feki na zingeweza kuhatarisha afya za akina mama yakiwemo na maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na fangasi ambao ni hatari kwa afya ya uzazi.

Alisema kati ya magonjwa ambayo ambayo mwanamke angeweza dkutumia bidhaa hizo ni pamoja na UTI ambayo wadudu hushambulia mfumo wa mkojo hatimaye kwenye viungo vya ndani vya uzazi.

Alisema daktari aliyethibitisha hilo alisema kuwa athari za maambukizo hayo ni mbaya kwani huweza kuambukiza haraka na hata wakati mwingine huleta mitafaruku ndani ya familia kwani huambukiza haraka wakati wa kufanya tendo la ndoa.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment