Rais wa Pakistan Huchinja Mbuzi Mweusi Kila Siku ili Asirogeke

Friday, January 29, 2010 / Posted by ishak /


Rais wa Pakistan, Asif Ali Zardari huchinja mbuzi mweusi mmoja kila siku ndani ya nyumba yake ili kujilinda na macho ya watu wenye husda na pia kujilinda na uchawi.
Msemaji wa rais wa Pakistan ameliambia gazeti la Dawn kuwa mbuzi hao huchinjwa katika misingi ya sadaka ambapo nyama hugaiwa kwa maskini ili kujipatia baraka za mungu na kuepukana na mabalaa.

"Umekuwa ni utaratibu wa kawaida wa Zardari kutoa sadaka ya nyama ya mbuzi. Amekuwa akifanya hivi kwa muda mrefu sana", alisema msemaji huyo wa rais, bwana Farhatullah Babar.

Mamia ya mbuzi wameishachinjwa ndani ya nyumba ya Zardari tangia alipoapishwa kuwa rais wa Pakistan mwezi septemba mwaka 2008, liliripoti gazeti la Dawn.

Inasemakana kuwa Zardari amekuwa akifanya hivyo kutokana na mambo kutomwendea vizuri katika uongozi wake.

Zardari aliingia madarakani baada ya kuuliwa kwa mkewe, waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Benazir Bhutto mwishoni mwa mwaka 2007.

Zardari anakabiliwa na misukosuko katika uongozi wake kutokana na upinzani wa kisiasa, kutetereka kwa uchumi na pia kutokana na vita dhidi ya wanamgambo wa kiislamu wanaowasapati Taliban.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment