Mwanaume Mwingine Apata Mimba, Kujifungua Mwezi Ujao

Tuesday, January 26, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume wa nchini Marekani ambaye alizaliwa kama mwanamke kabla ya kubadili jinsia yake kuwa mwanaume anatarajia kujifungua mtoto wa kiume mwezi ujao.
Scott Moore mwanaume wa nchini Marekani ambaye alizaliwa kama mwanamke anatarajia kuwa mwanaume wa pili wa nchini Marekani kupata mimba na kujifungua mtoto.

Scott anatarajia kujifungua mtoto wa kiume mwezi ujao.

Mume wa Scott ambaye naye alizaliwa mwanamke kabla ya kubadilisha jinsia na kubadilisha nyeti zake, anatarajia kuwa pembeni ya Scott wakati wa kujifungua.

Scott amejibadilisha jinsia kuwa mwanaume lakini alikubaliwa kuolewa kisheria na Thomas kwa kutumia cheti chake cha kuzaliwa ambacho kinamuonyesha kuwa yeye ni mwanamke.

Thomas yeye anahesabika mwanaume kwakuwa alibadilisha jinsia yake na kufanya operesheni ya kuuondoa uke na kuupandikiza uume.

Scott yeye bado hajafanya operesheni hiyo ya kuuondoa uke wake hivyo bado ana sehemu za siri za kike.

"Tunajua watu watatukosoa lakini sisi tuna furaha ya kupata mtoto na wala hatujisikii vibaya", alisema Scott mwenye umri wa miaka 30 ambaye alisema mtoto wao wamepanga kumpa jina la Miles.

Scott anasema kwamba alizaliwa kama mwanamke akipewa jina la Jessica na alianza kupata shauku ya kuwa mwanaume alipoanza kupevuka alipokuwa na umri wa miaka 11.

Scott aliendelea kusema kuwa wazazi wake awali walimpinga lakini baadae walimsaidia kutimiza nia yake ya kuwa mwanaume.

Alianza kumeza vidonge vya homoni za kiume alipokuwa na umri wa miaka 16 na wazazi wake walimlipia gharama za kuyaondoa matiti yake.

Scott anasema kuwa alishindwa kulipia gharama za operesheni ya kuutoa uke wake na kuupandikiza uume hivyo hadi leo bado ana sehemu za siri za kike.

Thomas kwa upande wake yeye alifanikiwa kufanya operesheni ya kuuondoa uke na kuupandikiza uume mwaka jana.

Scott alipata ujauzito baada ya kupandikizwa mbegu za kiume za mwanaume ambaye yuko karibu na familia hiyo.

Scott anasema kuwa ana mpango wa kumzaa mtoto wake kwa njia ya asili.

"Hatukutaka kuwashtua watu watakapoona mwanaume anajitokeza kuja kujifungua", alisema Scott akielezea jinsi walivyomtafuta daktari wa kumzalisha.

Scott anasema kuwa hawakumpata kirahisi daktari huyo kwani madaktari wengi walikuwa wakikwepa kuonana naye na hata kumpa matibabu.

"Tunataka kuwaonyesha watu kuwa watu waliobadilisha jinsia nao wanaweza kuanzisha familia zilizojaa upendo na furaha", alisema Thomas.

source nifahamishe