Afisa Magereza Atupwa Jela Kwa Kufanya Mapenzi na Mfungwa

Friday, January 29, 2010 / Posted by ishak /


Afisa magereza mwanamke wa jela moja nchini Uingereza amehukumiwa kwenda jela miezi 21 baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mfungwa ndani ya jela.
Lisa Harris, afisa magereza katika jela ya Pentonville jijini London, amehukumiwa kwenda jela miezi 21 kwa kufanya mapenzi na mfungwa ambaye anasubiria hukumu yake kwa kula njama ya kumwagia tindikali mpenzi wake wa zamani.

Lisa alikiri makosa matatu ya kujivinjari na mfungwa huyo mwanaume wakati wa kazi ndani ya jela hiyo ya wanaume.

Lisa mwenye umri wa miaka 28 anatuhumiwa kufanya mapenzi na mfungwa hatari Daniel Lynch ambaye alitupwa jela baada ya kumtuma mtu amwagie tindikali mpenzi wake wa zamani.

Daniel alimtuma mwanaume huyo amwagie mpenzi wake wa zamani tindikali ya sulphuric acid.

Daniel pia anakabiliwa na mashtaka mengine ya kumbaka mtangazaji wa taarifa ya habari, Katie Piper.

source nifahamishe