Madaktari Waukata Mguu wa Kushoto Badala ya Mguu wa Kulia

Tuesday, January 26, 2010 / Posted by ishak /




Wednesday, January 27, 2010 12:42 AM
Madaktari nchini Peru bila kutarajia waliukata mguu wenye afya badala ya mguu uliotakiwa kukatwa wenye maambukizi na walipogundua kosa lao waliumalizia kuukata mguu uliobaki hivyo kumwacha mgonjwa akiwa amepoteza miguu yake yote miwili.
Madaktari nchini Peru walijichanganya na kuukata mguu wa kushoto wa mwanaume mwenye umri wa miaka 86 badala ya kuukata mguu wake wa kulia ambao ulikuwa na maambukizi.

Mwanaume huyo alitakiwa kukatwa mguu wake wa kulia ili kuzuia maambukizi katika mguu wake kusambaa mwilini mwake.

"Nilishtuka sana niliponyanyua shuka na kuona madaktari wameukata mguu wake wa kushoto badala ya mguu wa kulia", alisema binti wa mwanaume huyo, Carmen Villanueva.

Carmen alisema kuwa madaktari katika mji wa Callao walikuwa wakimpatia matibabu baba yake tangia januri 4 mwaka huu kutokana na maambukizi aliyokuwa nayo katika mguu wake wa kulia.

Baada ya hali yake kuwa mbaya sana siku ya jumamosi, waliamua kufanya operesheni ya dharura kuukata mguu huo ili kuzuia maambukizi kusambaa mwilini mwake.

Baada ya kugundua makosa yao, madaktari waliamua kumfanyia operesheni nyingine mwanaume huyo siku iliyofuatia na kuukata mguu wake wa kulia uliotakikana kukatwa tangia awali na kumwacha mwanaume huyo akiwa amepoteza miguu yake yote miwili bila kutegemea.

Hospitali ya Sabogal Hospital ilisema imewasimamisha kazi kwa muda madaktari waliofanya operesheni hizo huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Waziri wa afya wa Peru, Oscar Ugarte alithibitisha tukio hilo na kusema "Bila shaka wanastahili kuadhibiwa.. ni tukio la kusikitisha na tumeanzisha uchunguzi".

Familia ya mwanaume huyo imepanga kufungua kesi mahakamani kuwashataki madaktari hao.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment