Haiti Yakabiliwa na Ukata wa Makaburi

Tuesday, January 26, 2010 / Posted by ishak /


Kufuatia tetemeko kubwa ka ardhi lililoikumba Haiti wiki mbili zilizopita, Haiti hivi sasa inakabiliwa na uhahaba wa makaburi ya kuwazika maelfu ya watu waliofariki kutokana na tetemeko hilo la ardhi.
Tetemeko kubwa ka ardhi la ukubwa wa 7.0 lililoikumba Haiti wiki mbili zilizopita, limesababisha uhaba wa makaburi ya kuwazika maelfu ya watu waliofariki kutokana na tetemeko hilo.

Watu zaidi ya 150,000 wanahofiwa kufariki kwenye tetemeko hilo la ardhi.

Mamia ya watu wamezikwa kwenye makaburi ya pamoja lakini bado idadi kubwa ya maiti zimezagaa kwenye mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo Port au Prince.

Maafisa wa shughuli za mazishi wamesema kuwa wamekuwa wakiwazika watu watatu watatu katika kila kaburi moja.

Mamia ya maiti zingine ambazo zimezagaa mitaani inasemaka zimekuwa zikichomwa moto.

Idadi kamili ya watu waliofariki kutokana na tetemeko hilo la ardhi imekuwa ni vigumu kupatikana kutokana na ugumu uliopo katika zoezi la kuhesabu miili ya watu waliofariki.

Mamia ya watu waliofariki kutokana na tetemeko hilo, miili yao bado imefunikwa kwenye vifusi vya majengo yao huku zoezi la kuokoa watu waliofunikwa na vifusi likiwa limeishasitishwa.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment