Kucharazwa Bakora 101 Kwa Kupata Ujazito Baada ya Kubakwa

Tuesday, January 26, 2010 / Posted by ishak /


Msichana mwenye umri wa miaka 16 wa nchini Bangladesh amehukumiwa kucharazwa bakora 101 kutokana na ujauzito alioupata baada ya kubakwa.
Msichana mwenye umri wa miaka 16 wa nchini Bangladesh ambaye alipata mimba baada ya kubakwa, amekuhumiwa kucharazwa bakora 101.

Baba wa msichana huyo naye amepigwa faini ya pesa na pia ameonywa kuwa asipolipa faini basi familia yake itafukuzwa kwenye kijiji wanachoishi.

Taarifa zilizotolewa na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu zilisema kuwa msichana huyo baada ya kubakwa na mwanaume mwenye umri wa miaka 20, hakuripoti tukio hilo sehemu yoyote kwa kuhofia aibu ya kubakwa.

Baada ya tukio hilo, msichana huyo aliozeshwa haraka haraka kwa mwanaume mwingine lakini alipewa talaka wiki chache baadae baada ya kugundulika kuwa ni mjamzito.

Tukio la kubakwa kwa msichana huyo lilitokea kwenye wilaya ya Brahmanbaria mwezi aprili mwaka jana.

Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Bangladesh, Daily Star, msichana huyo ambaye jina lake liliwekwa kapuni, aliona aibu sana kuripoti polisi kuwa amebakwa.

Kesi yake ilibumburuka hadharani baada ya wazee wa kiislamu wa kijiji hicho kupitisha hukumu hiyo na kutaka msichana huyo atengwe mpaka wazazi wake watakapokubali adhabu hiyo itekelezwe.

Mbakaji wake alikamatwa lakini alisamehewa baada ya kuomba msamaha mbele ya wazee wa kijiji.

"Nataka haki itendeke, ameniharibia maisha yangu", alinukuliwa msichana huyo akiliambia gazeti la Daily Star.


source nifahamishe