Rais wa Afrika Kusini Amtia Mimba Binti wa Rafiki Yake

Sunday, January 31, 2010 / Posted by ishak /


Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ambaye ana jumla ya wake watatu amemtia mimba binti wa rafiki yake wa karibu.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amepata mtoto wa 20 baada ya kumtia mimba binti wa rafiki yake wa karibu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini.

Gazeti la Sunday Times la Afrika Kusini limeripoti leo kuwa Zuma alimpachika ujauzito Sonono Khoza ambaye ni binti wa Irvin Khoza, mmiliki wa timu ya Orlando Pirates.

Sonono mwenye umri wa miaka 39 alijifungua mtoto wa rais Zuma mwenye umri wa miaka 67 mwezi oktoba mwaka jana.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, baba yake Sonono amehuzunishwa sana na kitendo cha Zuma kumtia mimba binti yake.

Khoza aliiambia familia yake kuwa anahisi amesalitiwa na Zuma ambaye alikuwa akimchukulia kama rafiki yake wa karibu sana.

Gazeti hilo liliendelea kusema kuwa mwezi disemba mwaka jana, wawakilishi wa rais Zuma waliitembelea familia ya Khoza katika mji wa Soweto na kujadiliana nao malipo ya kitamaduni ya kumzalisha mwanamke nje ya ndoa (inhlawulo).

Rais Zuma alikutana na Sonono na mama yake mwanzoni mwa mwezi huu kulijadili zaidi suala hilo.

Zuma hivi sasa anaishi na jumla ya wake watatu na amewahi kufunga ndoa jumla ya mara ya tano.

Mtoto wa Sonono amekuwa mtoto wa 20 katika idadi kubwa ya watoto wa rais Zuma.

source nifahamishe